• 1. Sisi Hatumo Miongoni Mwao Wanaosita na Kupotea kwa Sababu ya Dhambi Zetu (Yohana 13:1-11)
    Jan 15 2023

    Neno lote la Biblia ni fumbo kwa walimu wa uongo ambao hawajazaliwa tena upya. Kwa hiyo wanajaribu kulifafanua Neno la Mungu kwa namna yao wenyewe kwa mawazo yaliyoundwa na mwanadamu. Hata hivyo, wao wenyewe hawashawishiki kuamini kile wanachokifundisha. Kama matokeo ya hali hiyo, hata miongoni mwa wale wanaoamini katika Yesu, kuna wachache sana wenye uhakika wa wokovu wao.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 11 mins
  • 2. Kisitiri na Nguzo za Mahali Patakatifu (Kutoka 26:31-37)
    Jan 15 2023

    Nitapenda kutafakari juu ya maana ya kiroho iliyomo katika nguzo za Mahali Patakatifu na rangi za kile kisitiri chake. Hema Takatifu ambalo tunalizama hapa lilikuwa na vipimo vya mita 13.5 (futi 45) kwa urefu na mita 4.5 (futi 15) kwa upana, na lilikuwa limegawanywa katika vyumba viwili vilivyoitwa Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Ndani ya Mahali Patakatifu kulikuwa na kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba, na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kulikuwa na Sanduku la Ushuhuda na kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku lile.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 18 mins
  • 4. Pazia Ambalo Lilipasuliwa (Mathayo 27:50-53)
    Jan 15 2023

    Patakatifu pa Patakatifu palikuwa ni mahali ambapo Mungu aliishi. Na ni Kuhani Mkuu tu ndiye aliyeruhusiwa kuingia hapo mara moja kwa mwaka, katika ile Siku ya Upatanisho hali akiwa amebeba damu ya mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi la waisraeli. Kuhani Mkuu alifanya hivyo kwa sababu Patakatifu pa Patakatifu katika Hema Takatifu la Kukutania palikuwa ni mahali patakatifu sana ambao hakuweza kuingia mpaka awe na damu ya mwanasadaka, ambaye kwa huyo mikono iliwekwa juu ya kichwa chake ili kuyatoweshea mbali maovu ya wenye dhambi. Kwa msemo tofauti, hata Kuhani Mkuu hakuweza kuikwepa adhabu ya Mungu hadi baada ya kuwa amepokea ondoleo la dhambi zake kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kabla ya kuingia katika uwepo wa Mungu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr
  • 3. Wale Wanaoweza Kupaingia Patakatifu pa Patakatifu (Kutoka 26:31-33)
    Jan 15 2023

    Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni jengo dogo lililokunjwa na lililokuwa limefunikwa na aina nne za mapaa. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa limeundwa kutokana na vifaa mbalimbali—kwa mfano, kuta zake ziliundwa kwa mbao 48 za mti wa mshita. Kimo cha kila ubao kilikuwa ni mita 4.5 (dhiraa 10: futi 15), na upana ulikuwa sentimita 67.5 (dhiraa 1.5: futi 2.2). Mbao zote zilifunukwa kwa dhahabu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    33 mins
  • 5. Vitako Viwili vya Fedha na Ndimi Mbili kwa Kila Ubao wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-37)
    Jan 15 2023

    Hema Takatifu la Kukutania liliundwa kwa mbao 48; kulikuwa na mbao 20 kwa kila upande wa kusini na kaskazini, mbao sita ziliwekwa upande wa magharibi, na mbao mbili ziliwekwa katika kona mbili za nyuma. Kila ubao ulikuwa na kipimo cha mita 4.5 (futi 15) kwa urefu na takribani sentimita 67.5 (futi 2.2) kwa upana. Ili kila ubao uweze kusimama vizuri ukiwa umenyooka kulikuwa na vitako viwili vya fedha na ndimi mbili ambavyo vilifungamana pamoja vizuri. Hii inatuonyesha tena kuwa wokovu wa Mungu unapatikana kwa neema yake tu kwa imani katika Kristo.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 13 mins
  • 6. Mafumbo ya Kiroho Yaliyofichwa Katika Sanduku la Ushuhuda (Kutoka 25:10-22)
    Jan 15 2023

    Mada ya leo ni Sanduku la Ushuhuda. Sanduku la Ushuhuda lilikuwa na vipimo vya sentimita 113 (futi 3.7) kwa urefu, sentimita 68 (futi 2.2) kwa upana, na sentimita 68 (futi 2.2) kwa kimo chake, Sanduku hili lilitengenezwa kwa mti wa mshita na lilifunikwa kwa dhahabu safi. Ndani ya Sanduku kulikuwa na mbao mbili za mawe zilizokuwa zimeandikwa Amri Kumi na bilauri ya dhahabu iliyokuwa na manna, na baadaye iliwekwa ile fimbo ya Haruni iliyochipuka. Je, vitu hivi vitatu vilivyowekwa ndani ya Sanduku hili la Ushuhuda vinatueleza nini? Kwa kupitia vifaa hivyo, nitapenda kutoa ufafanuzi wa kina na wa upana kuhusiana na huduma tatu za Yesu Kristo. Hebu sasa na tuchunguze juu ya ukweli wa kiroho uliodhihirishwa katika vifaa hivi vitatu vilivyokuwa vimewekwa ndani ya Sanduku la Ushuhuda.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    46 mins
  • 7. Sadaka ya Ondoleo la Dhambi Inayotolewa Katika Kiti cha Rehema (Kutoka 25:10-22)
    Jan 15 2023

    Dhiraa ni urefu unaoanzia katika ncha ya kidole cha mkononi hadi kwenye kiwiko. Katika Biblia, dhiraa inakadiriwa kuwa na kipimo cha sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Urefu wa kiti cha rehema ulikuwa ni dhiraa mbili na nusu, na kwa hiyo kipimo hicho kinapo badilishwa katika vipimo vya kisasa, urefu huu unakuwa sawa na sentimita 113 (futi 3.7). Na upana wake ulikuwa ni dhiraa moja na nusu ambao ni sawa na takribani sentimita 67.5 (futi 2.2). Vipimo hivi vinatupatia sisi ule ufahamu wa kawaida juu ya kipimo cha kiti cha rehema.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    42 mins
  • 8. Meza ya Mikate ya Wonyesho (Kutoka 37:10-16)
    Jan 15 2023

    Meza ya mikate ya wonyesho ambayo ni moja ya vifaa vinavyopatikana ndani ya Hema Takatifu la Kukutania iliundwa kwa mti wa mshita na kisha ikafunikwa kwa dhahabu safi. Ilikuwa na vipimo vya dhiraa mbili (sentimita 90: futi 3) kwa urefu, dhiraa moja na nusu (sentimita 67.5: futi 2.2) kwa kimo, na dhiraa moja (sentimita 45: futi 1.5) kwa upana. Juu ya meza ya mikate ya wonyesho kulikuwa na mikate 12 ambayo iliwekwa pale wakati wote, na mikate hii iliweza kuliwa na makuhani tu (Mambo ya Walawi 24:5-9).

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    47 mins