• HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (II)

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (II)

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hakimiliki © 2008 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • 1. Sisi Hatumo Miongoni Mwao Wanaosita na Kupotea kwa Sababu ya Dhambi Zetu (Yohana 13:1-11)
    Jan 15 2023

    Neno lote la Biblia ni fumbo kwa walimu wa uongo ambao hawajazaliwa tena upya. Kwa hiyo wanajaribu kulifafanua Neno la Mungu kwa namna yao wenyewe kwa mawazo yaliyoundwa na mwanadamu. Hata hivyo, wao wenyewe hawashawishiki kuamini kile wanachokifundisha. Kama matokeo ya hali hiyo, hata miongoni mwa wale wanaoamini katika Yesu, kuna wachache sana wenye uhakika wa wokovu wao.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 11 mins
  • 2. Kisitiri na Nguzo za Mahali Patakatifu (Kutoka 26:31-37)
    Jan 15 2023

    Nitapenda kutafakari juu ya maana ya kiroho iliyomo katika nguzo za Mahali Patakatifu na rangi za kile kisitiri chake. Hema Takatifu ambalo tunalizama hapa lilikuwa na vipimo vya mita 13.5 (futi 45) kwa urefu na mita 4.5 (futi 15) kwa upana, na lilikuwa limegawanywa katika vyumba viwili vilivyoitwa Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Ndani ya Mahali Patakatifu kulikuwa na kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba, na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu kulikuwa na Sanduku la Ushuhuda na kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku lile.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 18 mins
  • 4. Pazia Ambalo Lilipasuliwa (Mathayo 27:50-53)
    Jan 15 2023

    Patakatifu pa Patakatifu palikuwa ni mahali ambapo Mungu aliishi. Na ni Kuhani Mkuu tu ndiye aliyeruhusiwa kuingia hapo mara moja kwa mwaka, katika ile Siku ya Upatanisho hali akiwa amebeba damu ya mbuzi wa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi la waisraeli. Kuhani Mkuu alifanya hivyo kwa sababu Patakatifu pa Patakatifu katika Hema Takatifu la Kukutania palikuwa ni mahali patakatifu sana ambao hakuweza kuingia mpaka awe na damu ya mwanasadaka, ambaye kwa huyo mikono iliwekwa juu ya kichwa chake ili kuyatoweshea mbali maovu ya wenye dhambi. Kwa msemo tofauti, hata Kuhani Mkuu hakuweza kuikwepa adhabu ya Mungu hadi baada ya kuwa amepokea ondoleo la dhambi zake kwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kabla ya kuingia katika uwepo wa Mungu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr

What listeners say about HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (II)

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.