• 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
    Jan 14 2023

    Uzio wa ua wa mstatiri wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na kipimo cha dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa ilihesabiwa kutokana na urefu unaoanzia katika kiwiko cha mkono hadi kwenye ncha ya kidole kama kiasi cha sentimita 45 au inchi 18 katika vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, kule kusema kuwa Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na dhiraa 100 kwa urefu kunamaanisha kuwa lilikuwa na mita 45 au futi 150; na kwamba upana wake ulikuwa dhiraa 50 maana yake ni kuwa lilikuwa na wastani wa takribani mita 22.5 au futi 75 kwa upana. Hivyo, hivi ndivyo vipimo ya Nyumba ambavyo Mungu aliishi miongoni mwa watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 35 mins
  • 2. Bwana Wetu Aliyeteseka Kwa Ajili Yetu (Isaya 52:13-53:9)
    Jan 14 2023

    Isaya alikuwa ni nabii aliyeishi karibu miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo hapa duniani. Pamoja na kuwa alitangulia kabla ya kuja kwa Yesu Kristo kwa miaka 700, na kwa sababu alifahamu mambo mengi kuhusu Masihi, Isaya alitabiri yote kuhusu jinsi Masihi atakavyokuja na jinsi atakavyofanya kazi yake ya wokovu kana kwamba alimuona Masihi kwa macho yake mwenyewe. Ukianzia Isaya 52:13 na kuendelea sura za 53 na 54, Isaya aliendelea kutabiri, kwa wazi na kwa kina, juu ya jinsi ambavyo Masihi atawaokoa wanadamu kutoka katika dhambi. Ni jambo la kushangaza sana kwamba Isaya alitabiri kwa usahihi kabisa kuwa Yesu Kristo atakuja hapa duniani na kuzichukua dhambi zote katika ubatizo wake, na kuimwaga damu yake Msalabani na hivyo kuuleta wokovu kwa wote. Na baada ya miaka 700 kupita tangu Isaya alipoutoa unabii wake, Yesu Kristo alikuja hapa duniani na akazitimiza kazi zake zote kwa usahihi kama ilivyotabiriwa na Isaya.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    46 mins
  • 3. Yahwe Mungu Aliye Hai (Kutoka 34:1-8)
    Jan 14 2023

    Hebu tuanze kwa kuangalia Kutoka 3:13-16: “Musa akamwambia Mungu, ‘Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakaniuliza ‘jina lake ni nani?’ Niwaambie nini?’Mungu akamwambia Musa, ‘MIMI NIKO AMBAYE NIKO;’akasema, ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli, ‘MIMI NIKO amenituma kwenu.’’ Tena Mungu akamwambia Musa, ‘Waambie wana wa Israeli maneno haya: ‘BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.’ Enenda ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, ‘BWANA Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, ‘Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri.’”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    27 mins
  • 4. Sababu Iliyomfanya Mungu Amuite Musa Kwenda Katika Mlima Sinai (Kutoka 19:1-6)
    Jan 14 2023

    Kifungu kikuu cha maandiko kinatoka katika Kutoka 19:1-6. Japokuwa kifungu hiki cha maandiko si kirefu, nina mambo mengi ya kuzungumza kuhusu kifungu hiki. Kutoka katika kifungu hiki, nitapenda pia kuzungumzia juu ya ukweli uliofunuliwa katika sura ya 19 na ile ya 25 katika kitabu cha Kutoka. Ilikuwa imeshapita miezi mitatu tangu watu wa Israeli walipotoroka kutoka Misri na kufika katika jangwa la Sinai. Mungu aliwafanya waweke kambi zao mbele ya Mlima Sinai, na kisha akamwita Musa kwenda juu mlimani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    33 mins
  • 5. Jinsi Ambavyo Waisraeli Walianza Kutoa Sadaka Katika Hema Takatifu la Kukutania: Msingi wa Kihistoria (Mwanzo 15:1-21)
    Jan 14 2023

    Ninaiheshimu na kuitamani sana imani ya Ibrahimu kama inavyoonyeshwa katika Biblia. Tunapoiangalia imani ya Ibrahimu, tunaweza kuona mateso na juhudi ya imani yake ambayo kwa hiyo alimfuata Yehova, na kwa jinsi hiyo hatuwezi kufanya lolote bali ni kuitamani imani ya Ibrahimu. Mungu alimbariki sana Ibrahimu, kama inavyoonyeshwa katika Mwanzo 12:3, ambapo Mungu alisema, “Nitawabariki wote watakaokubariki, Na nitamlaani yeyote atakayekulaani; na katika wewe jamaa wote wa dunia watabarikiwa.” Baraka hizi nyingi zinaonekana pia katika Mwanzo 15:1, ambapo Mungu alitamka kwa Ibrahimu kuwa “Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana”. Mungu alikuwa na upendo maalum kwa Ibrahimu kiasi kwamba Mungu alijiona kuwa ni Mungu wa Ibrahimu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    20 mins
  • 6. Ahadi ya Mungu Iliyothibitishwa Katika Agano Lake la Tohara Bado Inafaa na Ni Muhimu Kwetu (Mwanzo 17:1-14)
    Jan 14 2023

    Katika sura ya 17 ya kitabu cha Mwanzo, agano la tohara ambalo Mungu amelianzisha na kulithibitisha na Ibrahimu linatuonyesha sisi juu ya tohara ya kiroho ambayo kwa hilo dhambi zote zinaondolewa toka kwa waisraeli kwa kuiweka mikono yao juu ya mwanasadaka wa kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania na kwa jinsi hiyo walizipitisha dhambi zao kwa mnyama huyo wa sadaka ya kuteketezwa. Kwa maneno mengine, agano ambalo Mungu alilolianzisha na kulithibitisha na Ibrahimu lilikuwa ni wonyesho unaoonyesha juu ya sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa zitakazokuja baadaye. Ahadi ambayo Mungu aliifanya kwa Ibrahimu kwa tohara, kwamba atakuwa Mungu wake na Mungu wa wazawa wake, ilitabiri hali ikiliheshimu Hema Takatifu la Kukutania, kwamba wazawa wa Ibrahimu watazipitisha dhambi zao katika sadaka ya kuteketezwa kwa kuiweka mikono yao juu ya kichwa cha mwanasadaka. Ni lazima tutambue na tuamini kuwa hii inatuonyesha sisi kwa nyongeza kwamba katika kipindi cha Agano Jipya Yesu atazichukua dhambi zote za ulimwengu kwa ubatizo wake alioupokea toka kwa Yohana.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    27 mins
  • 7. Vifaa vya Ujenzi vya Hema Takatifu la Kukutania Vilivyoweka Msingi wa Imani (Kutoka 25:1-9)
    Jan 14 2023

    Mungu alimwamuru Musa kwenda juu katika Mlima Sinai na akampatia mtitiriko mzima wa Sheria yake. Kwanza kabisa, alimpatia Musa Amri Kumi: “Usiwe na miungu mingine ila Mimi; usijifanyizie sanamu kisha ukaziabudu; usilitaje bure jina la Bwana Mungu wako; ikumbuke siku ya Sabato na kuifanya kuwa takatifu; waheshimu baba na mama yako, usiue, usizini; usiibe; usimshuhudie uongo jirani yako; na usitamani mali ya jirani yako wala chochote alichonacho.” Kwa nyongeza, Mungu aliwapatia sheria nyingine ambazo waisraeli walitakiwa kuzitunza na kuzifuata katika maisha yao ya kila siku: Hizo zilikuwa ni amri 613 na sheria za Mungu kwa jumla.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    2 hrs
  • 8. Rangi ya Lango la Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)
    Jan 14 2023

    Kuna tofauti za wazi kati ya imani ya wale waliozaliwa upya na ile ya wakristo wa mazoea: imani ya wale waliozaliwa upya inafahamu na kuamini kuwa Mungu amezifuta dhambi zao zote, na imani ya wakristo wa mazoea inamwamini Yesu kwa kuyategemea mawazo yao binafsi, ni kama suala la kidini tu. Pamoja na hayo wale wanaomwamini Mungu kama sehemu ya masuala ya kidini wanafanikiwa sana kiasi kuwa wale wanaohubiri ukweli halisi wanaumizwa moyo pale wanapowaona watu hawa wenye imani potofu wakiyaeneza mafundisho yao ya uongo huku wakifanikiwa. Wanaumizwa mioyo kwa sababu wanafahamu wazi kuwa Wakristo wengi sana wanaletwa katika dini hiyo ya uongo na udanganyifu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    2 hrs and 26 mins