• HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (I)

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (I)

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na ya Roho Mtakatifu tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, rangi za bluu, Zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho Mtakatifu, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika rangi za bluu, zambarau, na nyuzi nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hakimiliki © 2012 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
    Jan 14 2023

    Uzio wa ua wa mstatiri wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na kipimo cha dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa ilihesabiwa kutokana na urefu unaoanzia katika kiwiko cha mkono hadi kwenye ncha ya kidole kama kiasi cha sentimita 45 au inchi 18 katika vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, kule kusema kuwa Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na dhiraa 100 kwa urefu kunamaanisha kuwa lilikuwa na mita 45 au futi 150; na kwamba upana wake ulikuwa dhiraa 50 maana yake ni kuwa lilikuwa na wastani wa takribani mita 22.5 au futi 75 kwa upana. Hivyo, hivi ndivyo vipimo ya Nyumba ambavyo Mungu aliishi miongoni mwa watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 35 mins
  • 2. Bwana Wetu Aliyeteseka Kwa Ajili Yetu (Isaya 52:13-53:9)
    Jan 14 2023

    Isaya alikuwa ni nabii aliyeishi karibu miaka 700 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo hapa duniani. Pamoja na kuwa alitangulia kabla ya kuja kwa Yesu Kristo kwa miaka 700, na kwa sababu alifahamu mambo mengi kuhusu Masihi, Isaya alitabiri yote kuhusu jinsi Masihi atakavyokuja na jinsi atakavyofanya kazi yake ya wokovu kana kwamba alimuona Masihi kwa macho yake mwenyewe. Ukianzia Isaya 52:13 na kuendelea sura za 53 na 54, Isaya aliendelea kutabiri, kwa wazi na kwa kina, juu ya jinsi ambavyo Masihi atawaokoa wanadamu kutoka katika dhambi. Ni jambo la kushangaza sana kwamba Isaya alitabiri kwa usahihi kabisa kuwa Yesu Kristo atakuja hapa duniani na kuzichukua dhambi zote katika ubatizo wake, na kuimwaga damu yake Msalabani na hivyo kuuleta wokovu kwa wote. Na baada ya miaka 700 kupita tangu Isaya alipoutoa unabii wake, Yesu Kristo alikuja hapa duniani na akazitimiza kazi zake zote kwa usahihi kama ilivyotabiriwa na Isaya.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    46 mins
  • 3. Yahwe Mungu Aliye Hai (Kutoka 34:1-8)
    Jan 14 2023

    Hebu tuanze kwa kuangalia Kutoka 3:13-16: “Musa akamwambia Mungu, ‘Tazama, nitakapofika kwa wana wa Israeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,’ nao wakaniuliza ‘jina lake ni nani?’ Niwaambie nini?’Mungu akamwambia Musa, ‘MIMI NIKO AMBAYE NIKO;’akasema, ndivyo utakavyowaambia wana wa Israeli, ‘MIMI NIKO amenituma kwenu.’’ Tena Mungu akamwambia Musa, ‘Waambie wana wa Israeli maneno haya: ‘BWANA, Mungu wa baba zenu, Mungu Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenituma kwenu; hili ndilo jina langu hata milele, nalo ni kumbukumbu langu hata vizazi vyote.’ Enenda ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja, ukawaambie, ‘BWANA Mungu wa baba zenu, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amenitokea, akaniambia, ‘Hakika nimewajilieni, tena nimeyaona mnayotendewa huko Misri.’”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    27 mins

What listeners say about HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA: Taswira ya Wazi na ya Kina ya Yesu Kristo (I)

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.