• SURA YA 7-1. Utangulizi Kwa Sura ya 7
    Jan 13 2023

    Kwa kuutambua ukweli kuwa kabla ya ukombozi wake mwili wake ulikuwa umehukumiwa kifo na Sheria ya Mungu, basi ndio maana Mtume Paulo alilifanya ungamo lake kwa kuamini kuwa alikuwa ameifia dhambi katika Yesu Kristo. Kabla hatujakutana na haki ya Mungu—yaani kabla hatujazaliwa upya—sisi ambao tunamwamini Kristo tulizoea kuishi chini ya himaya na laana ya Sheria. Hivyo, ikiwa tusingekutana na Yesu ambaye ametuletea haki ya Mungu basi Sheria ingeendelea kututawala.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    19 mins
  • SURA YA 7-2. Kiini cha Imani ya Paulo: Ungana na Kristo Baada ya Kuifia Dhambi (Warumi 7:1-4)
    Jan 13 2023

    Je, umewahi kuona bunda la nyuzi zilizojisokota? Ikiwa unajaribu kuifahamu sura hii pasipo kuufahamu ukweli wa ubatizo wa Yesu ambao Mtume Paulo aliuamini, basi ni hakika kuwa imani yako itakuwa katika wakati mgumu kuliko hapo kabla.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    50 mins
  • SURA YA 7-3. Sababu Inayotufanya Tumsifu Bwana (Warumi 7:5-13)
    Jan 13 2023

    Ninamsifu Bwana ambaye ameniongoza hadi kuonana na ninyi watu wa Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu kwa kunibariki na kunifanya niishi maisha yenye furaha hadi leo hii. Mungu ameendelea kuwa pamoja nami na amekuwa akinihurumia ingawa kulikuwa na nyakati ambazo nilikuwa najisikia kukatishwa tamaa, nyakati ambazo nilikutana na magumu na kupata udhaifu ndani yangu katika vipindi mbalimbali. Mungu amekuwa makini na amekuwa upande wangu katika maisha yangu yote katika shida na katika furaha. Hakukuwa na wakati wowote ambapo Mungu aliniacha hata kwa sekunde moja.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    29 mins
  • SURA YA 7-4. Miili Yetu Ambayo Inautumikia Mwili Tu (Warumi 7:14-25)
    Jan 13 2023

    Sisi hatuwezi kufanya jambo lolote ikiwa Mungu hatendi kazi akiwa upande wetu. Mungu wetu anatutunza na anatusaidia. Hebu tuliangalie Neno la Mungu. Warumi 7:14-25 inatueleza sisi kuwa Mtume Paulo alijiona yeye mwenyewe kuwa anaishi katika mwili hali akiwa ameuzwa chini ya dhambi. Pia aligundua kuwa kwa sababu ya sheria mwili hauwezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kufanya dhambi muda wote atakapokuwa hai.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    32 mins
  • SURA YA 7-5. Mwili Unaitumikia Sheria ya Dhambi (Warumi 7:24-25)
    Jan 13 2023

    Biblia inatueleza sisi pia kuwa, “kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.” Na hizo ndio sheria zinazotutawala. Mioyo yetu imeumbwa kumpenda Mungu na kuupenda ukweli, lakini ni kawaida kwa mwili kuitumikia sheria ya dhambi. Neno la Mungu linatueleza sisi kuwa moyo unaitumikia injili na haki ya Mungu ilhali mwili unaitumikia dhambi tu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    39 mins
  • SURA YA 7-6. Tumsifu Bwana, Mwokozi wa Wenye Dhambi (Warumi 7:14-8:2)
    Jan 13 2023

    Wanadamu wote walirithi dhambi toka kwa Adamu na Hawa na wakafanyika kuwa mbegu ya dhambi. Hivyo sisi ni viumbe wenye dhambi. Kwa asili tunazaliwa kama uzao wa dhambi na hivyo tunajikuta ni viumbe wenye dhambi. Watu wote duniani hawawezi kufanya lolote zaidi ya kuendelea kuwa wenye dhambi kwa sababu ya baba yetu wa kwanza Adamu ingawa hakuna yeyote anayetaka kuwa mwenye dhambi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    45 mins
  • SURA YA 8-1. Utangulizi Kwa Sura ya 8
    Jan 13 2023

    Pengine sura ya 8 inaweza kuelezewa kuwa ni sura muhimu sana miongoni mwa sura kadhaa za kitabu hiki cha Warumi. Paulo anatufunulia jinsi ambavyo haki ya Mungu ilivyo ya kushangaza kwa kupitia mada mbalimbali ambazo zinapatikana katika kitabu hiki.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    6 mins
  • SURA YA 8-2. Haki ya Mungu, Utimilifu wa Hitaji la Sheria Kwa Mwenye Haki (Warumi 8:1-4)
    Jan 13 2023

    Warumi 8:1-4 inatueleza sisi juu ya aina ya imani ambayo wale walio katika Kristo wanayo. Siri ya kifungu hiki ni kwamba tunaweza kukutana na maagizo yote ya Sheria katika haki ya Mungu kwa imani yetu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    34 mins