• Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Agano Jipya linaanza na Injili Nne ambazo ni Mathayo, Marko, Luka, na Yohana. Injili zote Nne zilishughulika na ziliandika kikamilifu kuhusu huduma ya Yohana Mbatizaji. Hii ni kwa sababu huduma yake ni ya muhimu sana. Hatuwezi kudai kuwa tunaifahamu huduma ya Yesu Kristo pasipo uelewa wa huduma ya Yohana Mbatizaji. Kama ndivyo, basi tunaweza kujiuliza, "Je, huduma ya Yohana Mbatizaji iliandikwa katika Injili Nne kwa umuhimu kiasi hicho?" Hali akimzungumzia Yohana Mbatizaji, Yesu alisema, "Na ikiwa mnataka kukubali, yeye ndiye Eliya atakayekuja" (Mathayo 11:14). Hivyo, Yohana Mbatizaji alikuwa ni mtu aliyezaliwa katika dunia hii ili kuitekeleza huduma maalumu. Pia Yesu alisema, "Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka" (Mathayo 11:12). Hii ni kweli kwa sababu Yohana Mbatizaji alizaliwa katika dunia hii, na wakati alipombatiza Yesu Kristo, dhambi za ulimwengu zilipitishwa kwenda kwa Yesu. Hivyo, Yesu aliweza kuzibeba dhambi za ulimwengu mara moja. Kwa kuruhusu jambo kuwa hivyo, Bwana amewaruhusu wale wanaoamini katika huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kuingia Mbinguni kwa kupokea utakaso wa dhambi. Hii ndiyo maana iliyomo katika kifungu cha maandiko toka katika Injili ya Mathayo sura ya 11, aya ya 12-14. Je, unaamini kuwa injili ya maji na Roho ndiyo Ukweli? Ikiwa unaamini hivyo, basi hii ina maanisha kuwa unaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kikamilifu. Hata hivyo, Wakristo wengi ambao hawaifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji hawaufahamu ukweli wa injili ya maji na Roho, na kwa sababu hiyo wanaishi maisha yao ya kiimani kwa jinsi ya matamanio ya miili yao. Pamoja na kuwa hawana ufahamu, watu wa jinsi hiyo hawajaribu hata kuifahamu huduma ya Yohana Mbatizaji iliyoandikwa katika Injili Nne. Kwa sababu hiyo, huduma ya Yohana Mbatizaji imekuwa haiheshimiwi kwa muda mrefu hata miongoni mwa Wakristo wanaodai kumwamini Yesu. Pengine kwa sababu hii, ninaona kuna watu wengi siku hizi ambao hawavutiwi na huduma ya Yohana Mbatizaji. Hivyo, watu wanakawaida ya kuwashangaa wale wanaovutiwa na mada hii. Hii ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiitazama kwa mbali huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu kiubishi kwa muda mrefu. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hakimiliki © 2006 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • 1. Ni Lazima Uifahamu na Kuiamini Huduma ya Yohana Mbatizaji (Marko 1:1-2)
    Jan 24 2023

    Marko 1:2 inasema, “Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako.” Ndugu zangu waamini, unaweza kuipata haki ya Mungu ikiwa tu utatupilia mbali uelewa wa kale na kuifuata Biblia kadri Neno la Mungu linavyokuongoza. Hivyo, wakati unaposoma Neno la Mungu, ni lazima ulisome hali ukiwa umeyaacha mawazo na tamaa zako za mwili. Ni kwa kufanya hivyo tu ndipo unapoweza kutambua na kuamini katika mapenzi ya Mungu ambayo anataka kuyatimiza. Kanuni hiyo inatumika pia katika kifungu cha Maandiko cha leo. Ni pale tu utakapokuwa umeyaachilia mbali mawazo yako ya kimwili na kisha ukalifuata Neno la Mungu linapokuongoza ndipo unapoweza kufahamu kiusahihi huduma ya Yohana Mbatizaji na huduma ya Yesu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    35 mins
  • 2. Yohana Mbatizaji Hakushindwa (Mathayo 11:1-14)
    Jan 24 2023

    Ni huduma gani hasa ambayo Yohana Mbatizaji aliitimiza kabla ya Yesu? Wakristo wengi leo hii hawamfahamu vizuri Yohana Mbatizaji, hivyo wanatakiwa kupata mtazamo mpya kuhusu Yohana Mbatizaji ili waweze kumfahamu na kuikubali huduma yake kikamilifu. Sisi sote tunapaswa kuwa na ufahamu sahihi na kuukubali uhusiano kati ya huduma ya Yesu na ile ya Yohana Mbatizaji. Kwa kuufahamu uhusiano huu kikamilifu, basi unapaswa kwanza kulipokea ondoleo la dhambi kwa imani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 5 mins
  • 3. Yohana Mbatizaji, Aliyekuja Katika Njia ya Haki (Mathayo 17:1-13)
    Jan 24 2023

    Kifungu cha Maandiko cha leo kinatoka katika injili ya Mathayo 17:1-13. Kifungu hiki kinaeleza kuwa Yesu aliwachukua wanafunzi watatu, Petro, Yakobo, na Yohana na akawaongoza kwenda katika mlima mrefu sana. Jambo la kushangaza lilitokea kule mlimani. Musa na Eliya walishuka toka Mbinguni. Na mavazi ya Yesu yalibadilika yakang’aa na kuwa meupe na sura yake ikabadilika pia. Yesu alizungumza na Musa na Eliya. Petro alipoona hivyo, akazungumza katika hali kindoto, “Na tufanye vibanda vitabu: kimoja chako, kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya. Tunapenda kujenga vibanda vitatu na kuishi pamoja nawe.” Kisha wingu likawafunika na sauti ikasema, “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye!”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    47 mins

What listeners say about Uhusiano Kati ya Huduma Ya YESU na Ile Ya YOHANA MBATIZAJI Kama Ilivyoandikwa Katika Injili Nne

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.