• Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (II)

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (II)

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Wakristo wengi siku hizi wanaiamini nadharia ya kunyukuliwa kabla ya dhiki. Kwa kuwa wanaiamini nadharia hii potofu, inayowaeleza kuwa watanyakuliwa kabla ya kuja kwa ile Dhiki Kuu ya miaka saba, ndio maana wanaendelea kuishi maisha ya kidini ya kivivu yanayojengwa katika haki binafsi. Lakini kunyakuliwa kwa watakatifu kutatokea baada ya mapigo yatakayotokana na tarumbeta la saba, yaani hadi pigo la sita litakapokuwa limemiminwa- yaani, kunyakuliwa kutatokea baada ya kuonekana kwa Mpinga Kristo katikati ya machafuko ya kidunia, wakati ambapo watakatifu waliozaliwa tena upya watakuwa wameuawa kwa kuifia-dini, na wakati ambapo tarumbeta la saba litakapokuwa limeshapigwa. Ni wakati huo ndipo Yesu atakaposhuka toka mbinguni, na hapo ndipo ufufuo na kunyakuliwa kwa waliozaliwa tena upya kutakapotokea (1 Wathesalonike 4:16-17). Siku hii, kila mtu katika ulimwengu huu atakuwa amesimama katika njia panda kuhusiana na hatma yake ya milele. Watakatifu waliozaliwa tena upya kwa kuamini katika "injili ya maji na Roho" watafufuliwa na kunyakuliwa, kisha watakuwa warithi wa Ufalme wa Milenia na Ufalme wa Mbinguni wa milele, lakini wenye dhambi ambao hawakuweza kushiriki katika ufufuo huu wa kwanza watakutana na adhabu kuu ya mabakuli saba yatakayomiminwa na Mungu na kisha watatupwa katika moto wa milele wa kuzimu. Hivyo, ni lazima sasa uachane na nadharia potofu za kidini pamoja na tamaa na miiko potofu ya ulimwengu huu, na kisha uingie katika Neno la Mungu la kweli. Ninatumaini na kuomba ili kwamba kwa kusoma mfululizo wa vitabu vyangu juu ya injili ya maji na Roho, basi ninyi nyote mtabarikiwa kwa dhambi zenu zote kuoshelewa mbali, na kisha kuupokea ujio wa Bwana wetu mara ya pili pasipo hofu. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hakimiliki © 2002 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • SURA YA 8-1. Matarumbeta Yanayoyatangaza Mapigo Saba (Ufunuo 8:1-13)
    Jan 14 2023

    Ufunuo 8 inaeleza juu ya mapigo ambayo Mungu atayaleta juu ya dunia hii. Moja kati ya maswali ya msingi hapa ni kwamba watakatifu watahusishwa ama kutohusishwa katika kuteseka chini ya mapigo hayo. Biblia inatueleza kuwa watakatifu pia, watayapitia mateso ya matarumbeta saba. Kati ya mapigo saba, watakatifu watayapitia mapigo yote isipokuwa ni lile pigo la mwisho. Mapigo haya saba ya matarumbeta yanayoonekana katika sura hii ni mapigo halisi ambayo Mungu atayaleta duniani. Mungu anatueleza kuwa atauadhibu ulimwengu kwa mapigo ambayo yataanza kwa sauti za matarumbeta saba ya malaika.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    12 mins
  • SURA YA 8-2. Je, Mapigo ya Matarumbeta Saba ni Halisi?
    Jan 14 2023

    Katika Ufunuo 5 kunaonekana andiko liliwekwa mihuri saba, ambalo Yesu alilichukua. Hii ilimaanisha kwamba Yesu alipewa mamlaka yote na nguvu za Mungu, na kwamba atauongoza ulimwengu kwa mujibu wa mpango wa Mungu kuanzia hapo na kuendelea. Ufunuo 8 inaanza kwa kifungu hiki, “Hata alipoifungua muhuri ya saba, kukawa kimya mbinguni kama muda wa nusu saa. Nami nikawaona wale malaika saba wasimamao mbele za Mungu, nao wakapewa baragumu saba.” Hivyo, Yesu anaifungua muhuri ya saba, kisha anatuonyesha vitu vitakavyokuja.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    37 mins
  • SURA YA 9-1. Pigo Toka Shimo Lisilo na Mwisho (Ufunuo 9:1-21)
    Jan 14 2023

    Kile kitendo cha Mungu kumpatia malaika ufunguo wa shimo la kuzimu lisilo na mwisho maana yake ni kwamba aliamua kuleta pigo la kutisha kama kuzimu kwa mwanadamu.
    Shimo lisilo na mwisho linafahamika kuwa ni kuzimu, maana yake ni sehemu ya kina kisicho na mwisho. Mungu atalifungua shimo hili la kuzimu ili kuleta mateso kwa Mpinga Kristo atakayekuwa akiishi duniani pamoja na wafuasi wake, na kwa wale wote wanaosimama kinyume dhidi ya wenye haki. Malaika wa tano alipewa ufunguo wa kulifungua shimo hili la kuzimu. Hili ni pigo la kutisha sana ambalo linatisha kama kuzimu inavyotisha.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    14 mins

What listeners say about Komentare na Mahubiri Juu ya Kitabu cha Ufunuo - JE, NYAKATI ZA MPINGA KRISTO, KUFIA-DINI, KUNYAKULIWA NA UFALME WA MILENIA ZINAKUJA? (II)

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.