• 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
    Jan 24 2023

    Wigo wa mstahili wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa moja ulikuwa ni urefu unaoanzia katika kiwiko cha mtu hadi katika ncha ya kidole, takribani sawa na sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, wigo wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni dhiraa 100 maana yake ni kwamba ulikuwa na urefu wa mita 45, na kule kusema kwamba urefu wake ulikuwa ni dhiraa 50 maana yake ni kuwa upana wake ulikuwa takribani mita 22.5. Kwa hiyo, hivi vilikuwa ndivyo vipimo vya Nyumba ambayo Mungu aliishi kati ya watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 44 mins
  • 2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)
    Jan 24 2023

    Kifungu hiki kinaelezea juu ya nguzo, lango la pazia, mapazia ya kitani safi ya kusokotwa, mikanda, vishikizio, vikuku vya shaba, na vigingi vya shaba vya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni mahali ambapo Mungu alikaa. Kipimo cha huo ua wa mstatili ulikuwa ni takribani mita 45 (kwa upande wake wa kaskazini na kusini) kwa mita 22.5 (katika upande wake wa mashariki na magharibi). Kimsingi, Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na umbo dogo lililokuwa na paa la lililokunjwa mara nne. Kwa upande mwingine, ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni mpana kama uwanja wa wazi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 4 mins
  • 3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)
    Jan 24 2023

    Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kisha kuikinga damu yake, na kisha kuikabidhi damu hii kwa kuhani. Kuhani aliye katika zamu yake aliiweka damu hii ya mwanasadaka katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, aliyaweka mafuta na nyama ya mwanasadaka huyo juu ya madhabahu, kisha akavichoma vitu hivyo kama manukato mazuri kwa Bwana Mungu. Hata Kuhani Mkuu, ili aweze kupokea ondoleo la dhambi zake, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zake kwa mnyama huyo mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Hii ilikuwa ni sadaka ya upatanisho iliyokuwa ikitolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo ilitengenezwa kutokana na mti wa mshita na kisha kufunikwa kwa shaba, na sadaka hii ya ondoleo la dhambi ilitolewa baada ya tendo la kuiweka mikono juu ya mwanasadaka na kisha kuimwaga damu huyo mwanasadaka.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    45 mins
  • 4. Madhabahu ya Uvumba Ni Mahali Ambapo Mungu Anaitoa Neema Yake (Kutoka 30:1-10)
    Jan 24 2023

    Kama tungeliingia ndani ya Mahali Patakatifu, ambapo ni Nyumba ya Mungu, kitu cha kwanza ambacho tungelikiona ni kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho, na madhabahu ya uvumba. Madhabahu ya uvumba iliwekwa mbele ya lango la kuingia Patakatifu pa Patakatifu, mahali ambapo kiti cha rehema kilikuwa kimewekwa, yaani baada ya kukipita kinara cha taa na meza ya mikate ya wonyesho. Urefu na upana wa madhabahu hii ya uvumba ulikuwa ni dhiraa moja, wakati kimo chake kilikuwa ni dhiraa mbili. Katika Biblia, dhiraa ni takribani sentimita 45-50 kwa vipimo vya hivi sasa. Hivyo, madhabahu ya uvumba ilikuwa na mraba mdogo wenye vipimo vya takribani sentimita 50 kwa urefu na upana na sentimita 100 kwa kimo. Kama ilivyokuwa kwa madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, madhabahu ya uvumba pia ilikuwa na pembe katika zake nne za juu. Hali ikiwa imetengenezwa kwa mti wa mshita, madhabahu ya uvumba ilikuwa imefunikwa yote kwa dhahabu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    48 mins
  • 5. Maana ya Kiroho ya Vikuku vya Fedha Vilivyotumika Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 26:15-30)
    Jan 24 2023

    Mbao zote za Hema Takatifu la Kukutania mahali ambapo Mungu alikaa zilikuwa zimefunikwa kwa dhahabu. Mungu alimwambia Musa kutengeneza vikuku vya fedha ili kuushikiza ubao uweze uweze kusimama wima. Maana ya kiroho ya kuweka hivi vikuku vya fedha chini ya kila ubao ni kama ifuatayo. Katika Biblia, dhahabu ina maanisha ni imani ambayo haiwezi kubadilika kutokana na wakati. Kule kusema kwamba hivi vikuku vya kushikiza viliwekwa dhini ya ubato uliokuwa umefunikwa kwa dhahabu maana yake ni kwamba Mungu ametupatia karama mbili ambazo zinatuhakikishia wokovu wetu. Kwa maneno mengine, ina maanisha kwamba Yesu ameukamilisha wokovu wetu toka katika dhambi kwa kubatizwa na kuimwaga damu yake.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 7 mins
  • 6. Kiti cha Rehema (Kutoka 25:10-22)
    Jan 24 2023

    Ndani ya Hema Takatifu la Kukutania kulikuwa kumegawanyika katika sehemu kuu mbili: Mahali Patakatifu na Patakatifu pa Patakatifu. Kulikuwa na pazia kati ya sehemu hizo mbili, na Sanduku la Ushuhuda lilikuwa nyuma ya pazia hili na ndani ya Patakatifu pa Patakatifu. Mfuniko wa Sanduku la Ushuhuda unajulikana pia kwamba ni kiti cha rehema.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    43 mins
  • 7. Vikombe Vya Mapambo Kwa Injili ya Maji na Roho (Kutoka 25:31-40)
    Jan 24 2023

    Kifungu hiki kinaelezea juu ya kinara cha taa cha Hema Takatifu la Kukutania. Leo nitapenda kuelezea juu ya maana ya kiroho ya vikombe hivi vya mapambo, maua na taa. Mungu alimwamuru Musa kutengeneza kwamba mhimili wa taa ili kutengeneza kinara cha taa cha dhahabu. Hivyo, kitu cha kwanza kilichofanyika ilikuwa ni kutengeneza huo mhimili, kisha baada ya huo mhimili yaliunganishwa matawi pembeni yake. Kila upande wa huo mhimili kulitengenezwa matawi matatu, kisha katika kila tawi kulikuwa na mabakuli matatu mfano wa ua la lozi, kisha vikombe vya mapambo na maua vilitengenezwa. Vivyo hivyo, taa saba ziliwekwa juu ya matawi hayo ili kuuangaza. Hivyo kinara cha taa kiliweza kuangaza vizuri kabisa ndani ya Patakatifu pa Patakatifu pamoja na vyombo vyake vya ndani.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    56 mins
  • 8. Maana za Kiroho Zilizofichika Katika Mavazi ya Kuhani Mkuu (Kutoka 28:1-43)
    Jan 24 2023

    Leo tutakwenda kuangalia juu ya maana za kiroho zilizofichika katika mavazi ya Kuhani Mkuu. Haruni alipaswa kuyavaa mavazi haya pamoja na watoto wake. Kwa kupitia mavazi haya ya Kuhani Mkuu tutaweza kutambua kwa imani juu ya mpango wa Mungu ambao umetuokoa toka katika dhambi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    56 mins