• HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Je, tunawezaje kuupata ukweli uliofichika katika Hema Takatifu la Kukutania? Ni kwa kuifahamu injili ya Maji na Roho tu, ambayo ni kiini cha kweli cha Hema Takatifu la Kukutania, ndipo tunapoweza kufahamu kwa usahihi jibu la swali hili. Kwa kweli, nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa kama zilivyodhihirishwa katika lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania zinatuonyesha kazi za Yesu Kristo katika kipindi cha Agano Jipya ambazo zimemuokoa mwanadamu. Kwa njia hii, Neno la Agano la Kale la Hema Takatifu la Kukutania na Neno la Agano Jipya yanahusiana kwa karibu sana kama vile ilivyo kwa nyuzi za kitani safi ya kusokotwa. Lakini, kwa bahati mbaya ukweli huu umefichwa kwa muda mrefu kwa kila mtafuta ukweli katika Ukristo. Alipokuja hapa duniani, Yesu Kristo alibatizwa na Yohana Mbatizaji na akamwaga damu yake katika Msalaba. Bila ya kuifahamu na kuiamini injili ya maji na Roho, hakuna kati yetu anayeweza kamwe kupata ukweli uliofunuliwa katika Hema Takatifu la Kukutania. Hivyo ni lazima tujifunze na kuuamini ukweli huu wa Hema Takatifu la Kukutania. Sisi sote tunahitaji kutambua na kuamini juu ya ukweli uliodhihirishwa katika nyuzi za bluu, zambarau, na nyekundu, na kitani safi ya kusokotwa za lango la ua wa Hema Takatifu la Kukutania. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hakimiliki © 2002 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • 1. Wokovu wa Wenye Dhambi Unafunuliwa Katika Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-21)
    Jan 24 2023

    Wigo wa mstahili wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa na dhiraa 100 kwa urefu. Katika Biblia, dhiraa moja ulikuwa ni urefu unaoanzia katika kiwiko cha mtu hadi katika ncha ya kidole, takribani sawa na sentimita 45 kwa vipimo vya kisasa. Kwa hiyo, wigo wa ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni dhiraa 100 maana yake ni kwamba ulikuwa na urefu wa mita 45, na kule kusema kwamba urefu wake ulikuwa ni dhiraa 50 maana yake ni kuwa upana wake ulikuwa takribani mita 22.5. Kwa hiyo, hivi vilikuwa ndivyo vipimo vya Nyumba ambayo Mungu aliishi kati ya watu wa Israeli katika kipindi cha Agano la Kale.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 44 mins
  • 2. Nguzo za Ua wa Hema Takatifu la Kukutania (Kutoka 27:9-19)
    Jan 24 2023

    Kifungu hiki kinaelezea juu ya nguzo, lango la pazia, mapazia ya kitani safi ya kusokotwa, mikanda, vishikizio, vikuku vya shaba, na vigingi vya shaba vya ua wa Hema Takatifu la Kukutania. Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa ni mahali ambapo Mungu alikaa. Kipimo cha huo ua wa mstatili ulikuwa ni takribani mita 45 (kwa upande wake wa kaskazini na kusini) kwa mita 22.5 (katika upande wake wa mashariki na magharibi). Kimsingi, Hema Takatifu la Kukutania lilikuwa na umbo dogo lililokuwa na paa la lililokunjwa mara nne. Kwa upande mwingine, ua wa Hema Takatifu la Kukutania ulikuwa ni mpana kama uwanja wa wazi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    1 hr and 4 mins
  • 3. Madhabahu ya Sadaka ya Kuteketezwa Iliyotengenezwa Kwa Mti wa Mshita na Kufunikwa Kwa Shaba (Kutoka 38:1-7)
    Jan 24 2023

    Ili mwenye dhambi yeyote kati ya watu wa Israeli aweze kuondolewa dhambi zake, basi ilimpasa kuleta mnyama wa sadaka ya kuteketezwa katika Hema Takatifu la Kukutania, na kisha kuzipitisha dhambi zake juu ya mnyama huyo wa sadaka kwa kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mwanasadaka huyo, na kisha kuikinga damu yake, na kisha kuikabidhi damu hii kwa kuhani. Kuhani aliye katika zamu yake aliiweka damu hii ya mwanasadaka katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, aliyaweka mafuta na nyama ya mwanasadaka huyo juu ya madhabahu, kisha akavichoma vitu hivyo kama manukato mazuri kwa Bwana Mungu. Hata Kuhani Mkuu, ili aweze kupokea ondoleo la dhambi zake, basi alipaswa kuiweka mikono yake juu ya mnyama wa sadaka ya kuteketezwa na kisha kuzipitisha dhambi zake kwa mnyama huyo mbele ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa. Hii ilikuwa ni sadaka ya upatanisho iliyokuwa ikitolewa katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa ambayo ilitengenezwa kutokana na mti wa mshita na kisha kufunikwa kwa shaba, na sadaka hii ya ondoleo la dhambi ilitolewa baada ya tendo la kuiweka mikono juu ya mwanasadaka na kisha kuimwaga damu huyo mwanasadaka.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    45 mins

What listeners say about HEMA TAKATIFU LA KUKUTANIA (III): Ubainisho wa Injili ya Maji na Roho

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.