• Roho Mtakatifu akaaye ndani yangu - Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

Roho Mtakatifu akaaye ndani yangu - Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Katika Ukristo nyakati hizi, mojawapo ya mambo yanayozungumziwa mara nyingi ni kuhusiana na habari za "wokovu toka dhambini" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu". Hata hivyo ni watu wachache walio na ufahamu ulio sahihi wa mambo haya mawili, ingawa ukweli ni kwamba haya ni mabo mawili muhimu kuhusiana na maswala ya Ukristo. Mbaya ni nini, bado hatujaweza kupata maandiko yanayo tufunza kwa uwazi juu ya mambo haya yaliyo tajwa hapo juu. Wapo watunzi wa vitabu wa Kikristo walio wengi wakitukuza karama za Roho Mtakatifu au kuelezea maisha ya kujazwa na Roho. Lakini hakuna hata mmoja kati yao anaye thubutu kushughulika na swali la msingi,nalo ni "Kwa namna gani anaye amini ataweza kumpokea Roho Mtakatifu kwa uhakika?" Kwanini? Ukweli wa kushangaza ni kwamba hawajaweza kuandika kwa viwango vilivyo kamili kwa sababu hawakuweza kuwa na ufahamu ulio kamili juu ya hili. Kama vili Nabii Hosea alipo paza sauti na kusema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", kwa nyakati hizi si wakristo wachache wanao vutwa katika ushabiki wa kidini, wakitegemea kumpokea Roho Mtakatifu. Huamini kwamba wataweza kumpokea Kumpokea Roho Mtakatifu baada ya kufikia kiwango cha hisia kali na mashamusham. Lakini si swala la kutia chumnvi tukisema kwamba kinacho itwa imani na watu hawa ndicho kinacho fanya Ukristo udharaulike na hata kuonekana kama mojawapo tu ya dini mfano Shama (Shamanism), na ukereketwa wa aina hii unatoka na Shetani Mtunzi, Mchungaji Paul C. Jong huthubutu siku zote kutangaza ukweli. Hujihusisha na maswala yaliyo muhimu kwa kiwango cha kutosha, ambacho wengi wa watunzi wa vitabu vya kiroho wamekwepa kwa muda mrefu. Kwanza amefafanua maana ya "kuzaliwa upya mara ya pili" na "kupokea uwepo wa Roho Mtakatifu" na kuelezea uhusiano usio kwepeka kati ya mambo yaha mawili ya ngozo za msingi. Na ndipo basi akachukua maelezo ya kina kwa pamoja kuhusiana na Roho Mtakatifu, kuanzia "namna ya utambuzi war oho" kuelekea "namna ya kuishi maisha ya ujazo wa Roho". Kwa habari zaidi mwandishi anakushauri uchunguze yaliyomo katika kitabu hiki ambayo yamewekwa katika kurasa za tovuti hii. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hati miliki © 2012 na Hepzabah Publishing House
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • 1. Roho Mtakatifu Hufanya kazi kupitia ahadi ya Neno la Mungu (Matendo 1:4-8)
    Jan 13 2023

    Hapo mwanzo nilipatwa na tukio la kujiwa na miale ifananayo kama Roho Mtakatifu wakati wa maombi. Lakini miale hii haikudumu kwa muda, hivyo punde ilitoweka mbele ya kitita cha dhambi. Ingawa leo napenda kukuonyesha ukweli kuhusu Roho Mtakatifu ambaye atakaye kaa ndani yetu hata milele, si kwakupitia roho zidanganyazo ambazo hutambulika kwa dhambi, bali kupitia injili ya kweli. Roho Mtakatifu nitakaye mtambulisha kwako kwa kupitia ujumbe huu si kitu fulani unacho weza kupokea kwa maombi bali kupitia imani katika injili ya majina Roho tu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    16 mins
  • 2. Je, inawezekana mtu kumnunua Roho Mtakatifu kwa uwezo wake? (Matendo 8:14-24)
    Jan 13 2023

    Husika na somo kuu katika kifungu hiki, napenda kuleta ujumbe huu iwapo “mtu anaweza kumpokea Roho Mtakatifu ndani yake kwa kupitia juhudi binafsi”. Mitume katika nyakati hizo za Kanisa la kwanza waliweza kupokea nguvu toka kwa Mungu na kutumwa sehemu kadhaa naye. Yapo matendo ya miujiza kadhaa katika Kitabu cha Matendo, mojawapo likiwa kushuka kwa Roho Mtakatifu juu ya waumini pale Mitume walipowawekea mikono. Biblia inasema “Mitume walipowawekea mikono wale ambao hawakuwa wamempokea Roho Mtakatifu ingawa walikwisha mwamini Yesu, walipokea Roho Mtakatifu.”

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    57 mins
  • 3. Mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini? (Matendo 19:1-3)
    Jan 13 2023

    Aina gani ya Injili Paulo alihubiri? Alihubiri Injili ya ubatizo wa Yesu na damu yake. Matendo 19:1-2 inasema “Ikiwa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akiisha kupita kati ya nchi za juu akafika Efeso, akakutana na Wanafunzi kadhaa wa kadha huko akawauliza, Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Hata hivyo watu hawa walikuwa wamekwisha mwamini Yesu huku wakiwa wameweka kando maana ya ubatizo wa Yesu. Hawakujua juu ya Injili njema ambayo hupelekea kumpokea Roho Mtakatifu ndani. Na hii kupelekea Paulo kuuliza “Je, mlimpokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” lilikuwa swali geni kwa baadhi ya wafuasi. Watu wengine wangeliweza kuuliza “Je, una mwamini Yesu?” Lakini Paulo aliuliza swali katika njia isiyokuwa ya kawaida ili kwamba waweze kumpokea Roho Mtakatifu, ndani yao kwa kufanya upya imani zao katika Injili njema. Huduma ya Paulo ilikuwa ni kuhubiri Injili njema ya ubatizo wa Yesu kwa Yohana Mbatizaji.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    19 mins

What listeners say about Roho Mtakatifu akaaye ndani yangu - Njia ya tahadhari kwako katika kumpokea Roho Mtakatifu

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.