• Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (I)

  • By: The New Life Mission
  • Podcast

Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (I)

By: The New Life Mission
  • Summary

  • Injili ya maji na Roho ni haki ya Mungu! Maneno katika kitabu hiki yatatosheleza kiu ya moyo wako. Wakristo wa nyakati hizi wanaendelea kuishi pasipo kufahamu suluhisho halisi la dhambi za kila siku watendazo kila kukicha. Je, unafahamu juu ya haki ya Mungu? Nadhani utajiuliza mwenyewe juu ya swali hili na hatimaye kuamini juu ya haki ya Mungu ambayo imedhihirishwa kupitia kitabu hiki. Haki ya Mungu imekuwa ikiandamana na Injili ya maji na Roho. Hata hivyo kama ilivyo hazina yenye thamani imekuwa ikifichwa mbali na macho ya wafuasi wa washika dini wengi kwa miongo kadhaa. Namatokeo yake watu wengi wamekuwa wakitegemea na kujigamba juu ya haki zao binafsi badala ya ile haki ya Mungu. Kwa hiyo kanuni za Kikristo zisizo na maana zimetawala imani katika mioyo ya waumini wengi huku wakidhani kwamba ndizo zenye haki ya Mungu. Kanuni za kuchaguliwa toka asili, kuhesabiwa haki na utakaso wa awamu kwa viwango, ni mojawapo ya kanuni kuu za mafundisho ya wakristo ambayo yameleta tafrani za kimawazo na utupu ndani ya nafsi za waumini. Lakini sasa, wakristo wengi imewapasa kurudi na kuelewa upya juu ya Mungu, kujifunza juu ya haki yake na hatimaye kuendelea na imani iliyo na uhakika. "Bwana wetu aliye haki ya Mungu" atakupatia nafsi yako uelewa mkuu na kukuongoza katika amani. Mwandishi anapenda uhodhi baraka ya kuifahamu haki ya Mungu. Baraka ya Mungu iwe nanyi. https://www.bjnewlife.org/ https://youtube.com/@TheNewLifeMission https://www.facebook.com/shin.john.35
    Hati nakili © 2011 na Kampuni ya Uchapaji ya Hephzibah
    Show More Show Less
activate_Holiday_promo_in_buybox_DT_T2
Episodes
  • SURA YA 1-1. Utangulizi katika Kitabu cha Warumi Sura ya 1
    Jan 13 2023

    “Waraka wa Paulo Mtume kwa Warumi” unaweza kuchuliwa kuwa ni hazina ya Biblia. Inahusika zaidi na namna ya mtu awezavyo kupata haki ya Mungu kwa kuiamini Injili ya maji na Roho. Ukilinganisha Waraka kwa Warumi na ule Waraka wa Yakobo, wapo wanaouelezea huu wa kwanza kama “maneno mfano wa mrija wakufyonzea” Hata hivyo Yakobo ni neno la Mungu kama ilivyo Warumi.Tofauti pekee ni kwamba, katika Warumi ni wathamani kwa sababu unatoa mtazamo wa kijumla katika biblia, hali Yakobo uthamani wake nao upo katika neno ambalo linalowawezesha wenye haki kuishi kwa mapenzi ya Mungu.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    48 mins
  • SURA YA 1-2. Haki ya Mungu iliyo dhihirishwa katika Injili (Warumi 1:16-17)
    Jan 13 2023

    Paulo Mtume hakuionea haya Injili ya Kristo. Alitamka juu ya Injili. Hata hivyo, moja ya sababu ambayo watu wengi hulia ingawa wanamwamini Yesu ni kwa sababu ya dhambi. Pia ni kutokana na upumbavu wao katika kushindwa kuikubali haki ya Mungu. Tutaweza kuokolewa kwa kuamini haki ya Mungu na kuachana na haki zetu binafsi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    38 mins
  • SURA YA 1-3. Mwenye haki ataishi kwa Imani (Warumi 1:17)
    Jan 13 2023

    Je, wenye haki huishi kwa namna ipi? Kwa imani. Wenye haki huishi kwa imani. Ukweli ni kwamba neno “Imani” ni la kawaida, lakini ni neno kuu na muhimu katika Biblia. Wenye haki huishi kwa imani tu. Natumaini tutaweza kupata mwanga toka katika kifungu hiki kwa sababu tuna mwili na Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu. Tunajaribu kutafsiri maandiko mengi kwa mawazo yetu pasipo kujua maana kamili iliyo fichika katika Biblia ingawa tunaweza kuelewa katika hali ya kawaidia. Kwa pamoja tuna mwili na Roho. Hivyo, Biblia inasema kwamba sisi wenye haki tutaishi kwa imani kwa sababu tunaondoleo la dhambi.

    https://www.bjnewlife.org/
    https://youtube.com/@TheNewLifeMission
    https://www.facebook.com/shin.john.35

    Show More Show Less
    36 mins

What listeners say about Haki ya Mungu Inayofunuliwa Katika Kitabu cha Warumi - BWANA Wetu Aliyefanyika Kuwa Haki ya Mungu (I)

Average customer ratings

Reviews - Please select the tabs below to change the source of reviews.